HUDUMA YANGU

                                  Nilianza huduma yangu ya uimbaji wa nyimbo za injili mwaka   
                                   2007 mnamo mwaka 2009 nikatoa album yangu ya kwanza
                                   nikaendelea mpaka mwaka 2012 nimefanikisha kuiachia album
                                  yangu ya pili [2] inayokwenda kwa jina la
                                   "NIACHENI NIMFUATE YESU" ambayo ina nyimbo 9
                                   ipo katika mfumo wa audio cd,vcd,dvd nk. hii album inapatikana
                                   katika maduka yote ya cd hapa nchini tanzania ama wasiliana nami



soma na hapa umuelewe sarah mvungi na kama una maswali nipigie
 Nilianza huduma hii ya uimbaji miaka mingi, sana nikiwa bado shuleni na lianza kuimba nyimbo za asili ya wapare, na nilikuwa nacheza na kuimba nyimbo za kabila hilo la wapare. na niliendelea na kuimba.nikiwa naendelea kukua nilijiunga na kwaya ya kanisa romani katolick kule kisangara juu mwanga, na baadae nilipomaliza shule nilienda,Tanga kwa wazazi na nilikaa kwa mda kidogo na tena nikaondoka nikaenda kisangara juu na baadae nikachukuliwa na mjomba wangu kwenda Dar es salaam.nilianza maisha upya nikiwa Dar es salaam na nilijiunga tena na mziki katika kanisa la ukonga romani catolc,niliendelea,na baada ya hapo nilibadili dini na kuwa muisilamunilikaa ktk uisilamu kwa miaka kumi na mbili na nilikuwa na watoto na mwaka 2001nilianza maisha ya u singel  nianza kuishi peke yangu ni baada ya kuachana na aliyekuwa mume wangu,mwaka 2003 nilipata mtot wa kike ninayempenda sana hata ukinunua alibamu yangu hii ya niacheni nimfuate yesu utamuona nilishirikiana nane kuimba na mtot wangu wa kwanza ambae sasa ni mkubwa alishiriki ktk kucheza niwwimbo anaoupenda katika alibam yangu unaitwa EH MUNGU. ukiangalia huu wimbo utamuona mtoto wangu wa kiume hapo amevaa fulana ya Tanzania,niliokoka mwaka 2004 na ilikuwa ni muujiza maana hata namna niliokoka ilikuwa ni mujiza sana,niliokoka nikiwa na heng over nilikunywa sana pombe siku ya jumamosi,na jumapili ndio nikapata bahati ya kumpokea YESU nakwambia kama unasoma hapa tambua kuwa nampenda sana YESU.nilianza kuimba mwaka 2007 na wimbo wangu wa kwanza kabisa katika wokovu na binafsi  unaitwa TUNASAFIRI,huu wimbo niliutunga nikiwa ndani ya basi na hakika ulikuwa wimbo wangu wa kwanza,nilifanikiwa kumaliza alibamu moja ilikuwa inaitwa YESU ASANTE na sasa nimemaliza alibamu nyingine inaitwa NIACHENI NIMFUATE YESU ninapenda nikwambie kuwa usikose hii alibamu na kama unalo swali lolote niandikie uniulizenitakujibu amen

Napenda kuimba, na sasa naandaa alibamu yangu ya tatu kaa mkao wa kuingoea nitashirikiana na waimbaji kama bahati bukuku mdg wangu nampenda sana na pia nitashirikiana na martha mwaipaja,na Joseph Bienvenue

                                    "MUNGU AKUBARIKI"